Posted by On the spot Tz
5:05:00 PM
0
Yanga
ni kama imewazuga wapinzani wao TP Mazembe ya DR Congo baada ya kuamua
kurejea kwenye jiji la Antalya, Uturuki kwa ajili ya kambi huku ikipanga
kutua Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili.
Hiyo
ni siku moja tangu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha timu
hiyo Jerry Muro kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa timu hiyo
ingerejea jana Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
Yanga
inatarajiwa kuvaana na Mazembe Jumanne ijayo kwenye mechi ya Kombe la
Shirikisho Afrika wakiwa walifungwana MO Bejaia ya Algeria bao 1-0,
kabla ya kurejea Uturuki.
Meneja
wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema itarejea usiku wa saa saba wa
kuamkia Jumapili na moja kwa moja wataingia kambini kujiandaa na mchezo
huo.
Saleh
alisema, timu hiyo iliingia Uturuki jana saa 12:00 asubuhi wakitokea
Algeria kuvaana na MO Bejaia na mara moja kuanza maandalizi ya mchezo
huo pamoja na mshambuliaji mpya raia wa Zambia, Obrey Chirwa.
"Awali
tulikuwa tupo kwenye mipango ya kurejea Dar mapema kwa ajili ya kuanza
maandalizi ya mechi na Mazembe, lakini uongozi umebadilisha mpango na
badala yake tutarejea Uturuki kuendelea na maandalizi hayo.
"Timu
itarejea huko Dar majira ya usiku wa kuamkia Jumapili saa saba na moja
kwa moja tutaingia kambini kwa ajili ya mchezo huo, hivyo tukiwa huku
Uturuki, ratiba ya mazoezi tumeibadilisha kidogo kwa kufanya mazoezi ya
jioni pekee na siyo usiku kama mwanzoni tukijiandaa na mechi na MO
Bejaia.
"Hiyo
yote ni kuendana na hali ya Dar ambayo ni ya joto kali kama ilivyokuwa
huku kuna jua na joto kali, hivyo kocha kashauri tufanye mazoezi kwa
muda huo,"alisema Saleh.
Kwa
upande wa Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm alisema
anachokifanya ni kuwatengeneza kisaikolojia wachezaji baada ya kupoteza
mechi na MO Bejaia ili wasahau matokeo hayo yaliyopita.
"Siku
zote ninapomaliza mechi moja, tunasonga mbele na kujiandaa na mechi
nyingine inayofuata, hivyo tumeona makosa yetu tuliyofanya katika mechi
iliyopita na badala yake ninayafanyia marekebisho makosa yaliyotokea.
"Kikubwa
ninawasisitizia wachezaji wangu kutofanya makosa kama tuliyofanya
kwenye mechi iliyopita ambayo yalitugharimu kwa wapinzani wetu kuyatumia
makosa yetu na kutufunga, hivyo sitaki hayo yajitokeze tena mechi na
Mazembe,"alisema Pluijm.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Picha za Zari Hassan Akijiachia Kuonyesha Ujauzito Wake,,,,,,,,,,Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenz...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: