Posted by On the spot Tz
11:02:00 PM
0
Wagombea Urais marekani
Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhakikishia nafasi yake ya kuwa mgombea wa Republican, Gavana John Kasich wa Ohio alifanikiwa kumzuwia bilionea huyo mwenye kauli za kutatanisha kuwika kwenye jimbo lake.
Wapiga kura vijana kwenye jimbo hilo muhimu waliamua kumkataa Trump, ambaye amekuwa akijizolea umashuhuri kwa kauli zake dhidi ya wale anaowaita wageni, Waislamu na wahamiaji.
"Imekuwa dhamira yangu kuwafanya vijana wa nchi hii kumuangalia mtu na kuingia kwenye siasa, ingawa muda mrefu watu walinipuuza. Watu wa Ohio walikuwa wakisema: "Kwa nini hawamuiti?" Tunafahamu hayo, lakini tunapiga hatua moja baada ya nyengine na leo nawahakikishieni kuwa sitarudi nyuma kuelekea safari ya ofisi hii kubwa kabisa katika nchi," gavana huyo aliwaambia wafuasi wake.
Ushindi wa Kasich ni wa kwanza kwake tangu kura hizi za mchujo za jimbo kwa jimbo kuanza wiki sita zilizopita. Hata hivyo, sio tu kuwa Trump alishinda kwenye majimbo ya North Carolina na Illinois, bali pia Florida, jimbo la mpinzani wake, Rubio, ambaye sasa amelazimika kujiengua moja kwa moja kwenye kinyang'anyiro hicho, hivyo kuwaweka Trump na Seneta Ted Cruz kuwa washika bendera.
'Tsunami ya Kisiasa'
Akiyaaga mashindano hayo, Rubio alisema alikuwa amejaribu kujenga daraja katika nchi na katika chama baada ya kutekwa nyara na kupasuliwa na kampeni za uasi za Trump, ambaye anamlaumu kwa kuiletea Marekani kile alichokiita "tsunami ya kisiasa."
Kwa upande wa Democratic, Hillary Clinton ameshinda pia kwenye majimbo yote manne: Florida, North Carolina, Illinios na Ohio, na kumuwacha mbali hasimu wake, Bernie Sanders.
"Usiku huu ni wazi kabisa kwamba ni moja ya kampeni zenye mafanikio makubwa kabisa maishani mwetu. Rais ajaye ataingia Ikulu mwezi Januari, akae kwenye kiti chake na kuanza kufanya maamuzi ambayo yataathiri maisha ya kila mmoja wetu kwenye nchi hii, na hakika kwenye dunia nzima."
Ushindi wa jana wa Clinton ulikuwa mkubwa, huku kwenye jimbo kama Florida akijizolea asilimia 65 dhidi ya 33 za Sanders, na ni katika jimbo la Illinois tu ambako Sanders alishindwa kwa asilimia moja.
Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Picha za Zari Hassan Akijiachia Kuonyesha Ujauzito Wake,,,,,,,,,,Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenz...
No comments: