Posted by On the spot Tz
5:00:00 PM
0
MZAMILU YASSIN
Kiungo
mpya wa Simba, Mzamilu Yasin aliyetokea Mtibwa Sugar ametamba kuwa
suala la kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo halina tatizo na
wala hatishwi na uwepo wa Jonas Mkude katika nafasi hiyo.
Mzamilu
aliyesajiliwa hivi karibuni kwamkataba wa miaka miwili pia alieleza
atajitolea zaidi kuisaidia Simba msimu ujao ili irejee kwenye njia yake
na kukata kiu ya makombe klabuni hapo.
Mzamilu
amefunguka kuwa hatishwi na uwepo wa viungo wengi klabuni hapo akiwemo
Justice Majabvi, Said Ndemla, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto, Peter
Mwalyanzi na Mkude kwa kuwa yeye ni mpambanaji na anaiamini kazi yake.
“Nacheza
nafasi zote za viungo ila napenda zaidi namba nane, namheshimu Mkude na
viungo wengine Simba lakini nikiri kuwa sina hofu ya namba kwenye
kikosi cha kwanza kwa sababu hakuna kikosi utakachokwenda ukakosa
changamoto ila kwa kuwa naiamini kazi yangu, hilo litakuwa jepesi, sina
wasiwasi.
“Lakini
niseme pia nina imani kubwa Simba itafanya vizuri msimu ujao kutokana
na usajili wanaoendelea kuufanya, ukichanganya na wachezaji
tutakaowakuta itakuwa ni timu nzuri na nina imani viongozi pia
watajipanga vya kutosha kwa ajili ya kuipa mafanikio timu msimu ujao,”
alisema Mzamilu.

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: