Donald Trump, anayewania kuteuliwa na chama chake cha Republican kugombea urais wa Marekani na ambaye ni maarufu kwa maneno ya chuki dhidi ya Waislamu, hivi sasa anaonekana kuhaha kutafuta kura za Waislamu.
Gazeti la The Hill linaloandika sana habari za Baraza la Congress la Marekani limeripoti kuwa, Walid Phares, mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Donald Trump amekuwa akitumia kimya cha vyombo vya habari kuzungumza na kujaribu kuwashawishi Waislamu wanachama wa chama cha Republican pamoja na wanaharakati wahafidhina wenye asili ya Mashariki ya Kati nchini Marekani wamuunge mkono Donald Trump.
Juhudi za siri za timu ya uchaguzi ya Trump za kusaka kura za Waislamu zinafanyika katika hali ambayo mara kwa mara Donald Trump amekuwa akilaumiwa vikali kutokana na matamshi yake ya chuki dhidi ya Waislamu.
Miongoni mwa matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu yaliyotolewa na mwanasiasa huyo wa Marekani ni kutaka Waislamu wazuiwe kuingia Marekani na vile vile kitendo chake cha kutaka kuanzishwe kitengo maalumu cha kuwafanyia ujasusi Waislamu nchini humo.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply