Umoja wa Mataifa umesema kuwa, kitendo cha Sudan cha kukataa kumuongezea muda wa iqama na kibali cha kuishi afisa mmoja wa ngazi za juu wa umoja huo, kina maana ya kumfukuza nchini humo.
Shirika la habari la Ufaransa jana lilinukuu taarifa ya umoja huo ikisema kuwa, serikali ya Sudan imekataa kumuongezea muda wa iqama Ivo Freijsen, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu. Umoja wa Mataifa ulikuwa umeiomba Khartoum imwongezee afisa wake huyo muda wa miezi 12 mingine wa kuishi Sudan. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hatua hiyo ya Khartoum ni uvunjaji wa hati na makubaliano ya Umoja wa Mataifa.
Freijsen ambaye tangu mwezi Februari 2014 amekuwa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya haki za binadamu nchini Sudan, ni afisa wa nne wa ngazi za juu wa umoja huo kufukuzwa nchini humo katika kipindi cha miaka miwili iliiyopita.
Wakala mmoja wa uratibu wa masuala ya kibinadamu unaoundwa na mashirikia ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine nyingi zisizo za kiserikali zimeelezea kusikitishwa kwao na hatua ya serikali ya Sudan ya kumfukuza afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.
Afisa huyo amefukuzwa nchini Sudan miezi michache tu tangu nchi hiyo ifunge ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Tearfund na kuwafukuza viongozi watatu wa shirika hilo katika miezi ya hivi karibuni..
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply