Posted by On the spot Tz
4:13:00 AM
0

Leo Manchester United wanavaana na Crystal Palace katika mchezo wa fainali ya kombe la FA utakaopigwa kwenye uwanja wa Wembley.
United hawakuwa na msimu mzuri baada kuishia hatua ya makundi UEFA na kudondokea michuano ya EUROPA ambayo hata hivyo walitupwa nje na Liverpool, hivyo kombe la FA ni muhimu sana kwao ili kufuta machozi ya machungu waliyopata.
United pia wamekosa nafasi ya kufuzu kucheza UEFA mwakani baada ya kushika nafasi ya tano nyuma ya Leicester, Arsenal, Tottenham na Manchester City.

Hata hivyo wakati United ikiwa chini ya Sir Alex Ferguson, kombe la FA lilikuwa kama ziada tu hasa baada ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu, ukizingatia ya kwamba walikuwa wakishinda mara kadhaa kwa pamoja ubingwa wa ligi kuu na makombe mengine likiwemo FA.
Hivyo basi, United wameamua kwamba endapo watashinda ubingwa wa FA leo, kamwe hawatafanya ‘bus parade’ kwenye jiji la Manchester kwa kuwa si kitu chenye uzito mkubwa kwao.
Bus parade hufanywa na timu zinazochukua makombe mbalimbali ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuwaonyesha mashabiki kombe/makombe waliyochukua.

Tagged with:
MICHEZO KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: