Posted by On the spot Tz
7:17:00 AM
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.
Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.
Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.
Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.
Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.
Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.
Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
HABARI KITAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: