MJUE  ABBAS  PIRA  MCHEZAJI ANAEWIKA  ULAYA  JAPO  HAPATI NAFASI KATIKA TIMU YA TAIFA,,,,,,,,,,
On the spot Tz

NA TOM  MACHUPA  in mk dons london.


             ABBAS  GULLAM  PIRA  AKITOKA  UWANJANI  BAADA  YA  MECHI  KUMALIZIKA.
NI  KWELI  KWAMBA  TANZANIA  IMEJALIWA  KUWA  NA  VIPAJI  VINGI  TENA  VILIVYOPO  NJE  YA  NCHI  NA  HAKUNA  HATA  MTU  MMOJA  ANAYE  VIFUATILIA  HIVI  VIPAJI  VYA  VIJANA  HAWA  HIVI  KARIBUNI  KUNA  TAARIFA  ZILIVUMA  KATIKA  MITANDAO  YA  KIJAMII  NA  KUMTAJA  MMOJA  KATI  YA  VIJANA  AMBAO  WAPO  NJE  YA  NCHI  ANAYECHEZEA  TIMU  YA  CHELSEA  AMBAYE  NI  ADAM  NDITI  LAKINI  MPAKA  SASA  KIJANA  HUYO  SIJUI  HATMA  YAKE  ILIISHIA  WAPI. 
        SASA   LEO  NAKULETEA  MTU  AMBAYE  LABDA  ULIKUWA  HUMFAHAMU  HAPO  AWALI  LAKINI  NI  MCHEZAJI  MKUBWA  WA  KITANZANIA  ANAYEWIKA  HUKO  BARANI  ULAYA  ANAITWA  ABBAS  GULLAM  PIRA  KIJANA  HUYU  ALIWAHI  KUCHEZA  HAPA  TANZANIA  KWA  MUDA  MFUPI  SANA  AKIWA  NA  KLABU  YA  COASTAL  UNION   YA  TANGA.

                                  ABBAS  PIRA  AKIPEWA  MAELEKEZO  NA  KOCHA  WAKE.
UTAJIULIZA  PIRA  NI  NANI ? NA  KABLA  YA  KWENDA  KUCHEZA  VILABU  VYA  ULAYA  ALITOKEA  WAPI ? 
KIPA  HUYU  ALIANZA  SOKA  AKIWA  NA  KIKOSI  CHA  TIMU YA  SHULE  YA  SEKONDARI   POPATLALY  YA  JIJINI  TANGA  ALIYOSOMA  KUANZIA  MWAKA  2002  HADI  2005  BAADA  YA  KUMALIZA    KIDATO  CHA  NNE   KATIKA  SHULE  YA  SEKONDARI  POPATLALY, ALIPATA  NAFASI  YA KWENDA KUSOMA  NCHINI  UINGEREZA   AMBAKO  ALIJIKUTA  AKIJIUNGA  NA  TIMU  ZA  MITAANI.

ABBAS  PIRA  AKIWAPANGA  MABEKI  WAKE  VIZURI.
ALICHEZA  TIMU  ZA  MITAA  KWA  KIPINDI  KIREFU  SANA KABLA  YA  KUPATA  FURSA  YA  KUFANYA  MAJARIBIO  KATIKA  KLABU  YA  CHELSEA NA BIRMINGHAM CITY.

AMEFANYA  MAJARIBIO  CHELSEA  KWANINI  HACHEZI   NA HAKAI  HATA  BENCHI?
LICHA  YA  KUWA  NA  UWEZO  MKUBWA  SANA  LANGONI   ULIOFANYA  KUVUTIWA  NA  WATU  WENGI  LAKINI  HAKUFANIKIWA  KUSAJILIWA  KATIKA  KIKOSI  CHA  CHELSEA   KUTOKANA  NA  KUTOKUWA  NA  REKODI  KATIKA  TIMU  YA  TAIFA  YA  TANZANIA.

     "HATUA  YA  TANZANIA  KUSHINDWA  KUWEPO  KWENYE  NAFASI  70  ZA  MWANZO  ZA  VIWANGO  VYA  FIFA, PIA  NI PIGO   JINGINE  KWAKE  KWANI  ILIKUWA  VIGUMU  KUSAJILIWA  NA  TIMU  KUBWA"
 PIRA  PIA  AMEWAHIKUFANYA  MAJARIBIO  KWENYE  VITUO  VYA  SOKA  VYA  CV  YA  ENGLAND  PIA  AMECHEZA  TIMU  NYINGI  KAMA  MK DONS, COLCHESTER UNITED, LEYTON  ORIENT,  LAKINI  PIA  ANA  CHETI  CHA   FA  FEDERATION  HIVYO  ANARUHUSIWA  KUFUNDISHA  TEAM  ZA  UNDER  17  KOKOTE  DUNIANI.
MAISHA YA  PIRA  NJE  YA  UWANJA.
PIRA  ALIANZA  KUCHEZA  SOKA  KATIKA  TIMU  YA  MZAMBARAUNI  YENYE  MASKANI  YAKE  JIJINI  TANGA MWAKA  1994.
AKIWA  NA  TIMU  HIYO  NDIPO  KOCHA   JOSEPH  LAZARO ( KOCHA  MSAIDIZI  WA  NDANDA KWA  SASA) ALIMWONA  NA  KUMPELEKA  COASTAL UNION.
AKIICHEZEA  COASTAL  UNION, PIRA  ALIIWEZESHA TIMU  HIYO  KUTAMBA AKIWA  NA WACHEZAJI   WENGINE  MAHIRI  WAKIWEMO  JUMA  MGUNDA , MOHAMEDI  KAMPIRA , SAID  MHANDO , NYENDI  MPANGALA, MWARAMI SAIDI , DEO MASSANJA NA  SANDE  PETER.

onthespottz.blogspot.com

«
Next

Newer Post

»
Previous
Bunge Uganda Laimwagia Sifa Tanzania,,,,,,,,,,,

No comments:

Leave a Reply