Posted by On the spot Tz
6:30:00 PM
0

Yanga huenda ikashusha pumzi kidogo katika nafasi ya beki ya kulia kwani Juma Abdul ameanza mazoezi ya nguvu na jana Ijumaa asubuhi alicheza dakika 90 uwanjani.
Abdul
aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi
ya Azam FC hivi karibuni ambapo Yanga ilishinda mabao 3-1, siku
alipoumia nafasi yake ilichukuliwa na Mbuyu Twite.
Alitibiwa
na kupata nafuu lakini akajitonesha katika mchezo wa Taifa Stars na
Misri wa kufuzu Kombe la Afrika 2017 na tangu hapo hakuonekana uwanjani,
ambapo alikuwa akiuguza jeraha hilo.
Baada
ya kufanya mazoezi ya ufukweni kwa wiki nzima, jana Abdul alifanya
mazoezi ya uwanjani kwenye Uwanja wa Garden uliopo Vijana, Kinondoni
jijini Dar es Salaam ambapo alitumia dakika 90.
SALEHJEMBE ilimshuhudia Abdul akianza na zoezi la kukimbia akizunguka uwanja mara 20 kabla ya kucheza uwanjani.
Akizungumza
baada ya mazoezi hayo, Abdul alisema: “Nipo fiti kabisa na ninaweza
kucheza mechi na TP Mazembe, wiki nzima nilikuwa na programu ya mazoezi
ya stamina katika Ufukwe wa Coco.
“Leo (jana) ndiyo nimeanza kucheza uwanjani na nimetoka freshi kabisa na sina shaka hata nikipewa mechi ya Mazembe.”
Wakati wenzake wakiwa kambini Antalya, Uturuki, beki huyo alikuwa chini ya uangalizi wa Daktari Haroun Ally.
Yanga
itacheza na TP Mazembe, Jumanne ijayo mchezo wa Kundi A wa Kombe la
Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...


No comments: