Posted by On the spot Tz
2:34:00 AM
0
Baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta 'Popa' kukosa penalti katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri, baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Mzee Ally Samatta, amefunguka kuwa ilikuwa lazima akose penalti hiyo kutokaana na kukosea hesabu zake kabla ya kuamua kupiga.
Stars imepoteza matumaini ya kuweza kufuzu katika fainali hizo kwa mara ya pili baada ya mwaka 1980, kufuatia kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo huo uliopigwa Wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Mzee Samatta alisema ilikuwa lazima nahodha huyo kukosa penalti ile kutokana na kukubali kudanganywa kizembe na kipa wa Misri, Essam El Hadary.
“Nimesikitika Mbwana kukosa ile penalti lakini kwa upande wangu nilijua mapema lazima atakosa kwa sababu alikubali mapema kuongopewa na yule kipa (El Hadary), kutokana na kugundua mapema sehemu alipokuwa nataka kuleta mpira na ndiyo matokeo yake aliupaisha.
“Unajua hata kule Msumbiji yeye ndiyo alisababisha tukashindwa kufuzu baada ya kukosa penalti ya mwisho kwa mtindo kama ule wa kubadilisha maamuzi haraka kitu ambacho kinampa urahisi wa kipa kudaka na wakati mwingine kupaisha.
“Hata yeye mwenye amekiri kuwa yule kipa aligundua sehemu atakayopiga akazidi upande ule na matokeo yake kosa na tayari ameshanieleza kulipa faini yake ya Sh5000 kwa kosa la kukosa penalti yake,” alisema Mzee Samatta.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: