SAMATA  ALIMWA  KADI  YA  NJANO  WAKATI  GENK  IKIPOKEA  KICHAPO  CHA  3  -  1  DHIDI  YA  BRUGGE,,,

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amelimwa kadi ya njano timu yake KRC Genk ikifungwa mabao 3-1 na Club Brugge katika mchezo wa mchujo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji kuwania kucheza michuano ya Ulaya.
Mchezo huo wa ugenini uliofanyika Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge, Samatta alilimwa kadi hiyo dakika ya 76, ambayo inakuwa ya pili tangu ajiunge na timu hiyo Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.



Katika mchezo huo, kwa mara ya kwanza Samatta alicheza dakika zote 90 jahazi la timu yake likizama kwa mabao ya Waholanzi beki Stefano Denswil dakika ya 21, kiungo Ruud Vormer dakika ya 43 na kiungo Myahudi, Lior Refaelov dakika ya 60.
Bao pekee la Genk leo limefungwa na mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis dakika ya 89.
Samatta leo amecheza mechi ya 12 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
Katike mechi hizo, ambazo tano tu alianza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge mchezo wa kwanza.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply