
Posted by On the spot Tz
1:53:00 AM
0
KIUNGO wa kimataifa wa Zimbabwe, Thabani Scara Kamusoko (pichani kushoto) amewasifu wachezaji wenzake wawili wa Yanga, beki Juma Abdul Mnyamani na kiungo Haruna Fadhil Niyonzima kwamba wana uwezo mkubwa kisoka.
Kamusoko aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga SC baada ya kujiunga nayo kutoka Platinums FC ya kwao Julai mwaka jana, amesema Juma Abdul na Niyonzima, ambaye ni Nahodha wa Rwanda wana vipaji vikubwa.
“Nimecheza mpira kwa muda mrefu, lakini hawa wachezaji wawili Juma Abdul na Haruna Niyonzima na miongoni mwa bora niliowahi kucheza nao,”amesema Kamusoko.

Rasta huyo amesema wachezaji hao wana uwezo mkubwa kisoka na wanaweza kucheza popote duniani, zaidi ya Tanzania na Yanga.
“Hawa wawili ni wachezaji wazuri miongoni mwa wazuri niliowahi kucheza nao, nawatakia heri Mungu awasaidie waweze kucheza kwa miaka mingi”amesema.
Katika msimu wake wa kwanza tu Yanga, Kamusoko ametokea kuwa kipenzi cha wapenzi wa timu hiyo kutokana na msaada wake ndani ya kikosi cha wana Jangwani hao.
Pamoja na kucheza nafasi ya kiungo akiwa mpishi wa mabao mengi yanayofungwa na washambuliaji wa timu hiyo, Mzimbabwe mwenzake Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe, lakini naye Kamusoko amefunga mabao nane katika mechi 46.
Kesho, Kamusoko anatarajiwa kuichezea Yanga katika mechi ya 47 itakapomenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC inahitaji pointi saba katika mechi nne zilkizobaki ili kufikisha 72 na kutangaza ubingwa mapema, kwani haziwezi kufikiwa na timu nyingine.
Mechi nne za Ligi Kuu za Yanga zilizobaki zote ni za ugenini tupu kuanzia dhidi ya Stand United kesho, Ndanda FC mjini Mtwara, Mbeya City mjini Mbeya na Majimaji mjini Songea baadaye.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: