Rasi wa muda wa Brazil Michel Temer amesema kuna uwezekano kuwa atashikilia wadhifa huo hadi mwaka 2019.
Temer alichukua uongozi wa nchi hiyo baada ya rais Dilma Rousseff kusimamishwa kazi kwa muda wa siku 180 kufuatia uamuzi wa seneti. Hata hivyo iwapo Rousseff hatapatikana na kosa, atarejea tena kwenye wadhifa wake kama rais ndani ya miezi sita.
Lakini akihojiwa Temer alitoa kauli kana kwamba tayari kesi ya Rousseff imeamuliwa na hawezi tena kurejea madarakani.
Amesema, anataka kuirejesha nchi kwenye njia sahihi ndani ya miaka miwili na miezi saba ijayo.
Hata hivyo hakuondoa kabisa uwezekano wa kurejea kwa rais Rousseff.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply