Posted by On the spot Tz
12:37:00 AM
0
Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesisitizia umuhimu wa kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia ya mazungumzo tu.
Sanjari na kuonyesha masikitiko yake makubwa kwa raia wa Syria ambao kutokana na njama za maadui wa taifa hilo, wanapitia hali ngumu kimaisha, amezitaka pande husika katika mgogoro huo kukaa pamoja kwa mazungumzo. Papa Francis amesema kuwa, mazungumzo ndiyo njia pekee ya kufikiwa amani na usalama nchini Syria. Kadhalika kiongozi huyo wa kanisa Katoliki amesisitiza juu ya ulazima wa pande husika kuheshimu usitishaji vita. Hii ni katika hali ambayo Wizara ya Ulinzi ya Russia pia imetangaza kuwa katika kuendeleza mpango wa 'Ukimya wa Serikali' pande za Moscow na Washington kwa upande mmoja na kadhalika Damascus na wapinzani kwa upande wa pili, wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda wa siku mbili nyingine katika viunga vya mji wa Damascus. Mpango huo wa usitishaji vita ulianza tangu tarehe 30 mwezi uliopita wa April kwa muda wa masaa 24 katika eneo la Ghouta ya mashariki, huko mashariki mwa mji wa Damascus na masaa 72 katika maeneo ya kaskazini ya Latakia.
Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...


No comments: