Posted by On the spot Tz
1:29:00 PM
0
HEADLINES
- 4:04 PMShabiki wa Kweli
Home AZAM HABARI MOTOMOTO HABARI ZA NYUMBANI LIGI KUU BARA AZAM FC WAIACHIA RASMI UBINGWA YANGA, WATOA SARE 2-2 NA JKT RUVU CHAMAZI
AZAM FC WAIACHIA RASMI UBINGWA YANGA, WATOA SARE 2-2 NA JKT RUVU CHAMAZI
Posted by: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE Posted date: 5/04/2016 06:34:00 PM / comment : 0
Kikosi Cha Azam Fc
AZAM FC imepoteza kabisa matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba, Yanga wajitahakikishia kutetea taji hilo Mei 10 wakishinda dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kwani watafikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Ligi Kuu.
Sare hiyo inaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na kufikisha 60 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kumaliza na pointi 69 ikishinda mechi tatu za mwisho, wakati Simba yenye pointi 58 inaweza kumaliza na pointi 70 ikishinda mechi zake nne zilizobaki.
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Selemani Kinungai wa Morogoro aliyesaidiwa na washika vibendera Lulu Mushin na Shaffih Mohammed wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Azam walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mabao hayo yalifungwa na pacha kutoka Ivory Coast, kiungo Kipre Michael Balou dakika ya 31 na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 37.
Kipindi cha pili, JKT Ruvu inayofundishwa na gwiji wa soka nchini, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ilibadilika na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili.
Alianza Saad Kipanga kufunga kwa penalti dakika ya 56 kabla ya Najim Magulu kufunga la pili dakika ya 72.
Kikosi cha Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Abdallah Kheri, David Mwantika/Said Mourad dk46, Himid Mao, Kipre Balou/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk80, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk64, John Bocco na Kipre Tchetche.
JKT Ruvu; Madenge Ramadhani, Hamisi Seif, Omar Kindamba, Paul Mhidze, Renatus Morris, Nashon Naftali, Abdulrahman Mussa/Samuel Kamuntu dk46, Hassan Dilunga, Najim Magulu, Mussa Juma na Saad Kipanga/George Minja dk89.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...


No comments: