Posted by On the spot Tz
1:08:00 AM
0
KOCHA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Stanley Okumbi amemuita mzaliwa wa Hispania, Ismail Said Athuman Gonzalez anayechezea klabu ya CD Las Palmas ya La Liga na Bruce Kamau wa Melbourne City ya Ligi Kuu ya Australia.
Wawili hao wataorodheshwa katika kikosi cha awali kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Tanzania mwishoni mwa mwezi huu.
Gonzalez, mzaliwa wa Hispania kwa baba mama Mspanyola na baba Mkenya tayari amekubali mwaliko huo na anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Harambee Stars kambi itakapoanza.
Kwa sasa, Mkenya huyo anacheza kwa mkopo klabu ya Cacereno ya Ligi Daraja la Kwanza, Segunda nchini Hispania.
Ismail Said Athuman Gonzalez akiwa kazini na timu yake Las Palmas katika La Liga
Kamau aliyezaliwa Kenya kabla ya kuhamia na wazazi wake Australia akiwa ana umri wa miaka minne, bado hajaamua achezee nchi ipi kutokana na zote Australia na Kenya kumuhitaji.
“Nafikiri ni muhimu kuwaangalia wachezaji wote waliopo, wakiwemo hawa wawili,” amesema Okumbi.
“Mazungumzo na Gonzalez yamekwenda vizuri sana, wakati Kamau bado hajafanya maamuzi kwa sababu na kule wanamtaka pi. Lakini tuna matumani ya kuwapata wote kwa ajili ya mchezo ujao wa kirafiki," amesema kocha huyo.
Bruce Kamau wa Melbourne City ya Ligi Kuu ya Australia.
Kenya inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi kujiandaa na mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Kongo nyumbani Juni 5.
Kabla ya kucheza na Tanzania Mei 29, Harambee Stars itacheza na Sudan.
onthespottz.blogspot.com
Tagged with:
MICHEZO KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...




No comments: