Posted by On the spot Tz
10:44:00 PM
0
Bayern Munich imeng’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani Munich, Ujerumani.
Atletico Madrid imesonga kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa bao la ugenini baada ya ushindi wa bao 1-0 ikiwa nyumbani Madrid.
Kusonga mbele kwa Atletico Madrid, maana yake Kocha Pep Guardiola ambaye anaondoka kwenda kujiunga na Manchester City, ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Bayern.
Mechi ilikuwa ngumu na tamu kuangalia na wenyeji walianza kupata bao katika dakika ya 31 kupitia Xabi Alonso.
Lakini Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico kabla ya Robert Lewandowski kuongeza la pili.
Kila timu ilikosa penalti wakianza Bayern kupitia Thomas Muller na upande wa Atletico, Fernando Torres naye akakosa, makipa wa timu zote wakiwa mashujaa kwa kuzipangua.
Atletico Madrid inasubiri mshindi kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City katika mechi itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Tagged with:
MICHEZO KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam,,,,,,,Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za b...
-
Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star, Jijini Dar Baada ya Kukutwa Kimejaa Makopo ya MIKOJO na KINYESIUKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako w...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: