YANGA  KAMA  LEICESTER  YAITUNGUA  STAND  UNITED  KWAO,,
MPIRA UMEMALIZIKA: FULL TIME

STAND UNITED 1-3 YANGA  

Dakika ya 90+3: Muda wowote mchezo utamalizika. 

Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 3 za nyongeza. 

Dakika ya 86: Mchezo unaendelea kwa kasi.

Tambwe anacheza faulo, anapata kadi ya njano. 

Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Salum Telela ameingia Mbuyu Twite. 

Dakika ya 82: Maguri anapiga penalti na kufunga, Stand wanapata bao moja

MAGURIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII 

Kamusoko alimchezea faulo, Seleman Kassim wa Stand mwamuzi akaweka penalti. 

Dakika ya 81: Stand wanapata penalti.

Dakika ya 69:Kamusoko anapiga shuti kali lakini linatoka hatua chache kutoka langoni.
  
Dakika ya 75: Yanga wanafanya mabadiliko, Ngoma anatoka anaingia Matheo.

Dakika ya 70: Stand waapata kona, wanapiga lakini inatoka nje. 

Mashabiki wa Yanga wameanza kupagawa kwa mabao matatu mpaka sasa. 


Dakika ya 63: Tambwe anafunga bao kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Simon Msuva. 

TAMBWEEEEEEEEEEEEE 

Dakika ya 60: Maguri anakimbia na mpira pembeni ya uwanja, anaingia katikati ya uwanja lakini juhudu zake zinashindwa kuwa nafaida baada yaYanga kuondoa hatari.  

Dakika ya 58: Mchezo bado haina kasi sana ila Yanga wanamiliki mpira muda mwingi. 

Dakika ya 52: Msuva anakosa nafasi ya wazi. 

Dakika ya 49: Watu wa usalama wanaenda upande ambapo mashabiki wanafanya vurugu, wanawatuliza na mchezo unaendelea. 

Dakika ya 48: Mchezo umesimama kwa muda kutokana na baadhi ya mashabiki kumfanyia fujo mwamuzi wa pembeni.
  
Dakika ya 46: Mchezo umeanza 

Kipindi cha kwanza kimekamilika, Yanga inaongoza mabao 2-0.
  
Zimeongezwa dakika mbili 

Dakika ya 45: Ngoma anafunga bao la pili baada ya kupitishiwa pasi nzuri kutoka katikati ya uwanja huku walinzi wa Stand wakijua ameotea.

Dakika ya 38: Mchezo umesimama, Ngoma anatibiwa. 

Dakika ya 37: Ngoma yupo chini ameumia lakini mchezo unaendelea. 

Dakika ya 35: Yanga wanafanya shambulizi lakini kipa wa Stand anaokoa.  

Dakika ya 30: Yanga wameanza kumiliki mpira muda mwingi
KOCHA WA STAND UNITED, LIEWIG


Dakika ya 24: Timu zote zinashambuliana kwa zamu. 

Dakika ya 20: Stand wanamiliki mpira muda mwingi sasa. 

Dakika ya 17: Elius Maguri anapiga shuti lakini linakuwa mchekea kwa kipa wa Yanga. 

Dakika ya 11: Yanga bado inaongoza bao 1-0, mchezo bado haina kasi licha ya Yanga kufunga bao la mapema.

Stand walipanda kufanya mashambulizi , Salum Telela wa Yangaakaunasa mpira akapiga ndefu, mshambuliaji wa Yanga, Donlad Ngoma akaunasa akakimbia nao na kwenda kufunga.

  

Dakika ya 2: Ngoma GOOOOOOO!!!!

Dakika ya 1: Yanga wanafanya mashambulizi. 

Mchezo umeanza
   
Timu zimeshaingia uwanjani, sasa ndiyo zinakaguliwa.
onthespottz.blogspot.com
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply