Posted by On the spot Tz
9:06:00 AM
0
Donald Trump, mgombea wa nafasi ya urais wa chama cha Republican nchini Marekani amezitaja siasa za kigeni za nchi hiyo kuwa ni msiba mkubwa na zilizokosa mwelekeo au mwanga wa stratijia.
Trump aliyasema hayo jana na kudai kuwa, endapo atachaguliwa kuwa rais wa Marekani atazifanya siasa za kigeni za nchi hiyo kuwa kipaumbele cha kwanza katika uongozi wake. Trump aliyasema hayo baada ya kupata ushindi katika mchuano wa ndani ya chama chake katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Amesisitiza kuwa siasa za kigeni za Marekani zitapewa nafasi kubwa katika utendaji kazi wake huku akidai kuwa, sasa umewadia muda wa kuzifanyia mabadiliko siasa hizo za kigeni nchini Marekani. Kadhalika amesema kuwa, katika kudhamini usalama wa Marekani, waitifaki wakei lazima wamudu gharama kubwa katika suala hilo. Amesema pia kwamba, mahusiano ya kibiashara baina ya Marekani na China lazima yafanyiwe mabadiliko na kuwepo usawa zaidi katika uga huo. Katika sehemu nyingine ametaka kutumiwa ukandamizaji zaidi katika kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi na kusisitiza kuwa kwa kuzingatia kuwa atakuwa mtekelezaji wa sheria kwenye utawala wake, basi atapanua wigo wa sheria ya kuwahoji watuhumiwa wa uhalifu.

Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: