Posted by On the spot Tz
9:10:00 AM
0
Duru za habari nchini Libya zimeripoti kuuawa raia 16 wa Misri kufuatia ufyatulianaji risasi na wafanya biashara ya magendo katika eneo la Bani Walid kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa habari hiyo raia hao wa Misri waliokuwa wanakusudia kuhajiri kinyume cha sheria kuelekea Libya na kisha Ulaya, wameuawa baada ya kupigwa risasi na wafanyabiashara ya magendo katika eneo hilo. Wakati huo huo, Ahmed Abu Zeid, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ameutaka ubalozi wa nchi yake huko Libya kufanya mawasiliano na viongozi wa eneo la Bani Walid na pia serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya ili kufahamu kiini cha kujiri tukio hilo. Abu Zeid pia ameutaka ubalozi huo kuchukua hatua za haraka ili kufahamu utambulisho wa wahanga wa mauaji hayo na kuirejesha miili yao nchini kwao. Hii ni katika hali ambayo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler amelaani mauaji dhidi ya raia hao wa Misri na kutaka kufanyike uchunguzi wa haraka kubaini wahusika, kama ambavyo pia ametaka kurejeshwa utawala wa kisheria katika eneo la Bani Walid. Itafahamika kuwa raia wengi wa Misri wapo nchini Libya wakishughulisha na kazi mbalimbali. Wengi wa Wamisri hao wanafanya kazi za ujenzi nchini humo
Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...


No comments: