DEREVA NA ABIRIA USIPOVAA HELMENT  WOTE NI WAHALIFU.
Na Tom  Machupa kutoka Tanga,

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga BENEDICT  WAKULYAMBA.


Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga BENEDICT  WAKULYAMBA amesema Jeshi la Polisi mkoani hapo linaendelea na oparesheni ya kukamata waendesha piki piki  maarufu kama BODA BODA  wasiovaa au kuwavalisha abiria wao kofia ngumu (HELMENT) wakati  wakiwa katika safari zao mbalimbali  lengo ni kuepusha vifo visivyo vya lazima kutokana na madereva hao kutokutii sheria za usalama barabarani.

Mwendesha  Boda Boda anayevunja sheria za usalama barabarani.

Kamanda WAKULYAMBA amesema  jukumu la kuvaa kofia ngumu si la dereva pekee bali hata abiria anatakiwa kuvaa kofia ngumu  ili awe na usalama wakati wote  ambao anatumia usafiri wa aina hio, Kwa yeyote ambaye hata heshimu sheria za Usalama Barabarani  jeshi la polisi litamchukulia hatua kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Aidha kamanda WAKULYAMBA amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa thelathini (30) ambao wamekaidi maagizo na kuvunja sheria za barabarani  ikiwemo kutokuvaa kofia ngumu (HELMENT) wakiwemo  madereva wa pikipiki (BODA BODA) na abiria  wao.

Mwendesha boda boda na Abiria wake wakiwa wamevaa kofia ngumu (HELMENT)

Kamanda  WAKULYAMBA  amewaomba wananchi wa Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi wanapohisi au kupata taarifa zozote za kihalifu ili Jeshi la polisi liweze kushughulikia ili Nchi na Mkoa kuwe na amani kwa ujumla.
Waendesha Boda boda wakiwa katika eneo lao la kazi.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply