TANGA FRESH WAPATA HATI YAO RASMI, WAMSHUKURU RAISI MAGUFULI.

Na  Tom  Machupa kutoka Tanga,

Meneja wa kiwanda cha Tanga Fresh MICHAEL KARATA akionyesha hati waliopokea kutokana na agizo la mhe.Rais mbele ya waandishi wa habari.

Agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI alilolitoa  siku ya jumapili tarehe 6/8/2017 wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha maziwa mkoani Tanga kijulikanacho kwa jina la Tanga Fresh kuhusu kuachiliwa kwa hati ya umiliki wa Ardhi ya kiwanda hicho  ambayo ilizuiliwa tangu mwaka 2011 limetekelezwa ikiwa ni siku ni siku tatu (3) tangu agizo hilo lilipo tolewa.

Akizungumza kwaniaba  ya  uongozi  wa Tanga freshi  meneja  mkuu  Michael Karata  amesema wanamshukuru mhe.Rais Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI kwakukubali  ombi  lao ambalo  lilikuwa  kikwazo cha kutoendeleza  uzalishaji wa kiwanda hicho. Pia meneja Karata amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela kwakumshawishi Raisi Magufuli kutembelea  kiwanda  chao kwani imewapa hamasa  kubwa na motisha ya kufanya kazi kwa bidii.

Meneja mkuu wa Tanga fresh MICHAEL KARATA.

Kwa  upande wake makamu mwenyekiti wa bodi ya wafugaji katika kiwanda cha Tanga fresh Hassan Mzee amesema wao kama wafugaji wanakila sababu ya kuhakikisha wanazalisha maziwa kwa wingi ili kukifanya kiwanda hicho kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuwahudumia watu wengi zaidi kuliko hivi sasa.

Makamu mwenyekiti wa bodi ya wafugaji  Hassan Mzee.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela hakusita kumshukuru Rais Magufuli kwa kuonyesha upendo wake kwa wananchi wa Tanga na kwakitendo cha kutatua matatizo yao kwa haraka pasipo kuchelewa,Aidha  mkuu wa mkoa martin shigela ameuomba Uongozi wa kiwanda cha Tanga Fresh kutumia hati hio kwa mipango waliojipangia tangu awali  ili kuenenda sawa na nia ya Rais katika kutengeneza Tanzania ya viwanda.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela Akiongea mbele ya waandishi wa habari.


Mkuu wa Mkoa pia ametumia nafasi hio kuwaambia wanahabari kuwa maagizo yote aliyotoa Rais Magufuli yatafanyiwa kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa kwa kufwata sharia na kanuni za nchi bila kumpendelea mtu yoyote.

Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kiwanda cha Tanga Fresh.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply