Wakimbizi Waislamu mjini Berlin, mji mkuu wa Ujerumani wameelezea matatizo yanayowakabili ukiwemo ukosefu wa misikiti na maeneo ya ibada kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Berlin ni moja ya miji mikubwa yenye idadi kubwa ya wakimbizi Waislamu ambao kwa mujibu wa serikali ya Ujerumani inafikia laki moja, suala ambalo litaifanya nchi hiyo kuingia gharama kubwa katika kuwahifadhi. Baada ya kuingia mwezi wa Ramadhani na kutokana na ukosefu wa maeneo yanayofaa kwa ajili ya kufanyia ibada kama vile misikiti, hali hiyo imewaweka pagumu zaidi wakimbizi hao Waislamu suala ambalo limewatia wasi wasi hata viongozi wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo kwa sasa Waislamu hao wanafanya ibada zao katika misikiti midogomidogo na michache sana mjini Berlin, suala ambalo linaonekana kuwa tatizo kubwa katika mwezi huu wa Ramadhani.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply