Kwa mara nyingine serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote ya wafuasi wa muungano wa CORD unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Raila Odinga, ili kushinikiza viongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kung'atuka madarakani.
Siku mbili ikiwa zimepita tokea kujiri maandamano ya wapinzani katika mji wa Kisumu yaliyosababisha mtu mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imepiga marufuku maandamano kama hayo nchini humo. Kwa mujibu wa wizara hiyo maandamano na machafuko yanayofanywa na wapinzani nchini humo yanakinzana na mapendekezo ya mahakama ya katiba ambayo ilikuwa imependekeza kudhaminiwa sheria za waandamanaji kwa upande mmoja, na kudhaminiwa usalama wa polisi kutoka kwa waandamanaji kwa upande wa pili. Kufuatia hali hiyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imeonya vikali juu ya mwendelezo wa matukio hayo ya upinzani. Kwa kipindi cha wiki sita sasa wapinzani nchini Kenya wamekuwa wakifanya maandamano yenye lengo la kushinikiza viongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kuondoka madarakani kwa kile kinachotajwa na wapinzani kuwa, tume hiyo haina tena itibari ya kusimamia uchaguzi mkuu wa mwakani nchini humo.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply