Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ujamali uliomo katika maneno ya Qur'ani Tukufu ni muujiza na ni mlango wa kuvutiwa na mafundisho aali na yenye maana pana ya aya hizo.
Ayatullah Ali Khamenei alisema hayo jana jioni kwenye jalsa iliyojaa nuru ya Qur'ani Tukufu, katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kubainisha kwamba: Utulivu wa kiroho na kidini, ni moja ya baraka za kuyaelewa vizuri mafundisho ya Qur'ani na kwamba utulivu huo huandaa mazingira ya kuongezeka imani ya watu kwa Mwenyezi Mungu na kwa nguvu Zake. Ayatullah Khamenei amesema kuwa, leo hii dunia inahitajia mno mafundisho ya Qur'ani Tukufu kuliko wakati mwingine wowote na kusisitiza kwamba: Lau kama maana pana ya aya za Qur'ani Tukufu watabainishiwa watu kwa lugha nyepesi na ya kisasa, bila ya shaka yoyote athari zake zitakuwa kubwa sana, na zitaandaa uwanja wa kupatikana maendeleo ya kweli ya mwanadamu kwa sababu heshima, nguvu, ustawi wa kidunia, kuimarika kimaanawi, kupanuka fikra na itikadi na kuwa na furaha na utulivu moyoni, yote hayo yanategemea namna tutakavyotekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Aidha ameelezea kufurahishwa kwake na namna vijana wa Iran wanavyozidi kujiimarisha ki-Qur'ani na kusema kuwa, kama mafundisho ya Qur'ani yatazingatiwa inavyotakiwa, bila ya shaka yoyote dunia itaokoka kutoka katika vimbunga vya matatizo yake yote ambayo ni mengi sana leo hii.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply