Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limewatuhumu askari wa kusimamia amani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwaua kiholela raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo imesema kuwa, askari hao wa Kongo DR ambao wanahudumu katika kikosi cha Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika (MINUSCA), waliwaua raia 18 wakiwamo wanawake na watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hata hivyo msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sanjari na kukadhibisha madai hayo amesema kuwa, wizara hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo dhidi ya askari wake. Romin Oba ameongeza kuwa, serikali ya Kinshasa inashirikiana na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwekwa wazi kadhia hiyo. Hii ni katika hali ambayo Stephan Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa akisema kuwa wafanyakazi wa Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch walizifanyia uchunguzi tuhuma hizo na kuwasilisha ripoti yao kwa viongozi wa kieneo. Ikiwa tuhuma hizo zitathibitishwa, basi zitawachafulia jina askari hao wa Kongo DR hasa kutokana na kuwa, kabla ya hapo pia askari wa nchi hiyo walituhumiwa kwa ubakaji na udhalilishaji wa kingono na kupelekea baadhi yao kurejeshwa nchini kwao.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply