Kamandi ya jeshi la Lebanon imetangaza kunasa na kusambaratisha mfumo wa kijasusi wa utawala haramu wa Kizayuni katika miinuko ya al-Barouk nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imeeleza kuwa, Jumanne ya jana askari wa nchi hiyo walifanikiwa kunasa vifaa hivyo katika miinuko ya mji huo wa al-Barouk na Ain Zhalta magharibi mwa nchi hiyo ambapo baada ya kuvinasa iliviharibu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifaa hivyo vya ujasusi ambavyo vilikuwa na mfumo wa kutuma picha na sauti, huku vikiwa na betri maalumu inayojichaji kila wakati, vinafanana na mawe ya eneo hilo suala ambalo ilikuwa vigumu kuvibaini. Kabla ya hapo Waziri wa Mawasiliano wa Lebanon, Boutros Harb alitangaza habari ya uepo wa mtandao wa ujasusi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel nchini humo. Sanjari na kutaka kubaini mtandao huo, alitangaza kuwa timu ya kiutalaamu nchini Lebanon kwa kutumia vifaa vya kisasa vya upelelezi, ilifanikiwa kunasa mtandao huo. Ujasusi unaofanywa na utawala wa Kizayuni ni kati ya harakati za kiuadui zinazofanywa na utawala huo kwa ajili ya kupenyeza na kukiuka haki ya kujitawala taifa la Lebanon. Mbali na ujasusi, utawala huo wa Kizayuni umekuwa ukikiuka kujitawala kwa taifa hilo kupitia meli zake za kijeshi na ndege za kivita.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply