Posted by On the spot Tz
6:24:00 PM
0
Baada
ya Yanga kuandika barua kwa Shirikisho la SokaTanzania (TFF), kuomba
ipate nafasi ya kumtumia Hassan Kessy, Simba wamelizungumzia suala hilo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema jeuri ndiyo
iliwaponza Yanga hadi suala kufikia lililopo sasa, hivyo wanatakiwa
kubadilika na kuwa waungwana na kuachana na majivuno.
Hans
Poppe 'raia' wa Iringa, amesema kama Yanga wanataka kumtumia Kessy,
waandike barua na iwe ya kiungwana, nao watajibiwa kiungwana.
"Sisi ni waungwana kweli, lakini kama mtu atakuwa anaonyesha dharau, anasema yeye ni timu ya wananchi basi tuone itakuwaje.
"Lakini
kama ni muungwana, basi anajibiwa kiungwana. Wao waandike barua na sisi
tutaona iko vipi. Kama wataandika na barua itaonekana si ya kiungwana,
basi wasubiri kumtumia baadaye baada ya pingamizi za usajili kupita,"
alisema Hans Poppe ambaye ni mwanajeshi mstaafu.
Yanga
ilishindwa kumtumia Kessy katika mechi yake dhidi ya Mo Bejaia nchini
Algeria baada ya blog hii kuandika kwamba kulikuwa na tatizo.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema kweli Yanga wameishawasilisha barua hiyo na wanategemea uungwana wa Simba kulimaliza hilo.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Picha za Zari Hassan Akijiachia Kuonyesha Ujauzito Wake,,,,,,,,,,Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenz...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: