HABARI ZAIDI
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya Bundesliga mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia vipindi vya startimes kwa wapenzi wa soka hapa nchini
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa kuwafahamisha wapenzi wa mpira kununua ving’amuzi na kujiunga na vifurushi ili kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa moja na startimes.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo kufanya mashindano ya uandishi wa mechi hiyo na kwa mshindi wa shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege kwenda moja kwa moja Ujerumani.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema wana mahusiano mazuri na bundesliga kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.
Meneja Uwendeshaji Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa huduma mpya ya malipo kwa wale wenye hali ya chini wanaweza kulipia siku moja king’amuzi cha Startimes kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.
Hata hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema kuwa ligi ya Bundesliga ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na ligi zingine duniani kwa kuwa na wachezaji bora
Nae Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa kampuni ya startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe 18-27 Agosti mwaka huu
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga
Picha ya Pamoja .
Na Tom
Machupa kutoka Tanga,
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga BENEDICT WAKULYAMBA.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Tanga BENEDICT WAKULYAMBA amesema Jeshi la Polisi mkoani hapo
linaendelea na oparesheni ya kukamata waendesha piki piki maarufu kama BODA BODA wasiovaa au kuwavalisha abiria wao kofia ngumu
(HELMENT) wakati wakiwa katika safari
zao mbalimbali lengo ni kuepusha vifo
visivyo vya lazima kutokana na madereva hao kutokutii sheria za usalama
barabarani.
Mwendesha Boda Boda anayevunja sheria za usalama barabarani.
Kamanda
WAKULYAMBA amesema jukumu la kuvaa kofia
ngumu si la dereva pekee bali hata abiria anatakiwa kuvaa kofia ngumu ili awe na usalama wakati wote ambao anatumia usafiri wa aina hio, Kwa yeyote
ambaye hata heshimu sheria za Usalama Barabarani jeshi la polisi litamchukulia hatua kwa
mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Aidha
kamanda WAKULYAMBA amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa
thelathini (30) ambao wamekaidi maagizo na kuvunja sheria za barabarani ikiwemo kutokuvaa kofia ngumu (HELMENT)
wakiwemo madereva wa pikipiki (BODA BODA)
na abiria wao.
Mwendesha boda boda na Abiria wake wakiwa wamevaa kofia ngumu (HELMENT)
Kamanda WAKULYAMBA
amewaomba wananchi wa Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
polisi wanapohisi au kupata taarifa zozote za kihalifu ili Jeshi la polisi
liweze kushughulikia ili Nchi na Mkoa kuwe na amani kwa ujumla.
Waendesha Boda boda wakiwa katika eneo lao la kazi.
Na Tom Machupa kutoka Tanga,
Meneja wa kiwanda cha Tanga Fresh MICHAEL KARATA akionyesha hati waliopokea kutokana na agizo la mhe.Rais mbele ya waandishi wa habari.
Agizo
la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI
alilolitoa siku ya jumapili tarehe
6/8/2017 wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha maziwa mkoani Tanga
kijulikanacho kwa jina la Tanga Fresh kuhusu kuachiliwa kwa hati ya umiliki wa
Ardhi ya kiwanda hicho ambayo ilizuiliwa
tangu mwaka 2011 limetekelezwa ikiwa ni siku ni siku tatu (3) tangu agizo hilo
lilipo tolewa.
Akizungumza
kwaniaba ya uongozi
wa Tanga freshi meneja mkuu Michael Karata amesema wanamshukuru mhe.Rais Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI kwakukubali ombi lao
ambalo lilikuwa kikwazo cha kutoendeleza uzalishaji wa kiwanda hicho. Pia meneja Karata
amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela kwakumshawishi Raisi Magufuli
kutembelea kiwanda chao kwani imewapa hamasa kubwa na motisha ya kufanya kazi kwa bidii.
Meneja mkuu wa Tanga fresh MICHAEL KARATA.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa bodi ya
wafugaji katika kiwanda cha Tanga fresh Hassan Mzee amesema wao kama wafugaji
wanakila sababu ya kuhakikisha wanazalisha maziwa kwa wingi ili kukifanya
kiwanda hicho kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuwahudumia watu wengi zaidi
kuliko hivi sasa.
Makamu mwenyekiti wa bodi ya wafugaji Hassan Mzee.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela hakusita kumshukuru Rais Magufuli kwa
kuonyesha upendo wake kwa wananchi wa Tanga na kwakitendo cha kutatua matatizo
yao kwa haraka pasipo kuchelewa,Aidha
mkuu wa mkoa martin shigela ameuomba Uongozi wa kiwanda cha Tanga Fresh
kutumia hati hio kwa mipango waliojipangia tangu awali ili kuenenda sawa na nia ya Rais katika
kutengeneza Tanzania ya viwanda.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela Akiongea mbele ya waandishi wa habari.
Mkuu
wa Mkoa pia ametumia nafasi hio kuwaambia wanahabari kuwa maagizo yote aliyotoa
Rais Magufuli yatafanyiwa kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa kwa kufwata sharia na
kanuni za nchi bila kumpendelea mtu yoyote.
Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kiwanda cha Tanga Fresh.
FULL TIME
Dakika ya 90 + 3: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inapata ushindi wa bao 1-0.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 88: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 86: Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Said Ndemla ambaye anapiga shuti kali linatoka nje.
Dakika ya 84: Simba wanamtoa John Bocco anaingia Laudit Mavugo.
Dakika ya 76: Manula yupo chini, inaonekana ameumia, anapatiwa matibabu. Mchezo umesimama kwa muda kisha ukaendelea.
Dakika ya 75: Rayon wanaamka na kupata kona, inapigwa lakini Manula anadaka.
Dakika ya 69: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kichuya ambaye aliushindwa kurejea uwanjani, nafasi yake inachukuliwa na mkongwe Mwinyi Kazimoto.
Dakika ya 68: Niyonzima anapiga pasi nzuri kwa Okwi lakini anashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 66: Shiza Kichuta ameumia mguu wakati anawania mpira na beki wa Rayon, anachechemea na kutoka nje.
Dakika ya 66: Mchezo una kasi kubwa, wachezaji wa Rayon wanaambiana kutulia kwa kuwa Simba wanashambulia kwa kasi.
Dakika ya 63: Simba wanapata kona, wanaanzisha kona fupi lakini walinzi wanaokoa.
Dakika ya 62: Simba wanaendelea kulishambulia lango la Rayon, wanapiga pasi nyingi, Niyonzima anashangiliwa kila napogusa mpira.
Dakika ya 59: Simba wanapiga pasi zaidi ya 1o, wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao, pasi ya mwisho inafika kwa Bocco anapiga shuti linatoka nje.
Dakika ya 55: John Bocco amefanya kazi nzuri, ameingia na mpira na kuwatoka walinzi wa Rayon lakini akashindwa kumalizia kazi nzuri aliyoifanya.
Dakika ya 52: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 48: Simba wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Simba wamefanya mabadiliko kadhaa, beki Mohamed Hussein ameingia pamoja na Haruna Niyonzima naye ameingia.
Dakika ya 45: Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, Simba inaongoza bao 1-0. Timu zimeingia vyumbani kupumzika.
Dakika ya 45 + 3: Rayon wanapata faulo, nje kidogo ya lango la Simba, wanapiga lakini inaokolewa.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa aiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 43: Beki wa Simba, Mbonde anaumia wakati akiokoa mpira.
Dakika ya 40: Okwi anajaribu kupambana kutafuta nafasi ya kupenya kwa beki wa Rayon lakini anazuiliwa.
Dakika ya 36: Mchezo unaendelea kwa timu zote kuwa kwenye presha kubwa licha ya kuwa ni mchezo wa kirafiki.
Dakika ya 35: Kotei anachezewa vibaya inakuwa faulo kuelekea kwa Rayon.
Dakika ya 30: Rayon wanawapunguza kasi Simba lakini mambo yanakuwa magumu.
Dakika ya 25: Kichuya anacheza vizuri, anatoa pasi kwa Okwi lakini anachelewa, walinzi wanaokoa.
Dakika ya 20: Mchezo una kasi kwa timu zote, Simba hawataki kuupozesha mchezo.
Dakika ya 16: Mchezo unaendelea kwa kasi, mashabiki wa Simba wameongeza nguvu ya kushangilia.
Dakika ya 15: Mohamed Ibrahim anaipatia Simba bao la kwanza, alipata pasi kutoka kwa Okwi, akaachia shuti mbele ya walinzi wawili wa Rayon Sports.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dakika ya 11: Simba ndiyo ambao wanamiliki mpira muda mwingi na wanatumia mawinga wao kufanya mashambulizi.
Dakika ya 6: Washambuliaji wa Simba wanaonekana kuanza kwa kasi, wanafika langoni mwa Rayon mara kadhaa.
Dakika ya 4: John Bocco ameshaangushwa chini mara mbili.
Dakika ya 1: Simba wameanza kwa kupigiana pasi na timu zote zinaonekana kusomana.
Mchezo umeanza.
Timu zote zimeshaingia uwanjani, kwa jili ya kuanza mchezo huu.
Kwa sasa wachezaji wanapasha misuli uwanjani. Idadi ya mashabiki ni wengi. Kikosi kitakachocheza leo dhidi ya Rayon Sports kimeshatangazwa, ndiyo hicho kilicho kwenye picha:
Kikosi cha wachezaji wa Simba watakaotumika msimu wa 2017/18 kimeshatajwa, wametajwa mchezaji mmoja mmoja ambapo walikuwa wakiingia uwanjani baada ya kutajwa jina la Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.
Leo ndiyo ile siku ambayo Wanasimba wengi walikuwa wakiisubiria kwa hamu, timu yao kuelekea msimu wa 2017/18 inatambulishwa. Shughuli hii inafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kipindi cha kwanza kimemalizika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Simba wanatoka kifua mbele wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mohamedi Ibrahim "MO" dk ya 16. Simba wanaonekana kuawala mpira zaidi eneo la katikati licha ya mshambuliaji mpya kutoka Azam JOHN BOCCO kutokuwa na mchezo mzuri kwa dakika hizi za kipindi cha kwanza..
Wenyeviti 50 wa Serikali za Mitaa wa CUF Mkoa wa Dar es Salaam wametangaza kuunga mkono uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF la upande wa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa vua uanachama wabunge wanne wa viti maalumu na madiwani wawili.
Wabunge waliovuliwa uanachama ni Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally, Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Raisa Abdallah Mussa, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.
Wakiwakilisha wenzao 36 wenyeviti 14 kutoka mitaa mbalimbali ya halmashauri za manispaa tano za Dar es Salaam wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhisha na kazi nzuri inayofanywa na Profesa Lipumba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake 14 mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi amewaambia wanahabari leo Jumanne Agosti 8 wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao wamebainika kukihujumu chama hicho.
"Tunamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF," amesema Shilingi
Mbali na hilo Shilingi amewataka watu wanaoingilia mgogoro wa chama hicho kuacha mara moja na kwamba mgogoro ni wa kikatiba na suala hilo lipo mahakamani muda si mrefu uamuzi utatolewa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Popular Posts
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Picha za Zari Hassan Akijiachia Kuonyesha Ujauzito Wake,,,,,,,,,,Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenz...