

Posted by On the spot Tz
12:31:00 AM
0
Wakati taarifa zikisema kuwa Kamati ya Ufundi ya Yanga inakusudia kukaa kujadili uwezekano wa kumrejesha Mrisho Ngassa, Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, anahaha kutaka kumsajili winga huyo katika kikosi chake.
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alisema winga huyo hana nafasi katika kikosi chake lakini taarifa za ndani zinasema kamati imepanga kukutana kujadiliana juu ya uwezekano wa kumrejesha kundini.
Nyota huyo aliyeondoka Yanga mwaka 2015 kuelekea Free States ya Afrika Kusini, hivi karibuni alivunja mkataba na klabu hiyo na sasa yupo jijini Dar.
Inasemekana Ngassa alilazimika kusitisha mkataba na klabu hiyo ya Afrika Kusini, lakini taarifa za kuaminika kutoka Yanga, kabla ya kufikia hatua hiyo aliwaomba kutaka kumalizia soka lake Jangwani.
Lakini Kocha wa City, Kinnah Phiri ambaye ndiye alimsainisha Free States baada ya msimu wa 2014/15, alisema kuwa yupo tayari kumpa mkataba hata leo kwani anamjua sana.
Hata hivyo, Mlawi huyo ameeleza hofu yake kuwa anaweza kumkosa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumlipa mshahara.
“Hata kama ni leo akinihakikishia yupo tayari kucheza Mbeya City, nawaagiza viongozi kumpa mkataba. Unajua mchezaji huru anaweza kujiunga na timu muda wowote hata kama usajili ukiwa umekwisha.
"Ngassa ni mchezaji aliyekamilika na ndiyo maana nilifanya juu chini asajiliwe Free States, japo sijajua ni nini kilitokea mpaka kufikia hatua ya kukatisha mkataba,” alisema Phiri.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.

On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.You May Also Like
Usikose Bundesliga msimu wa tatu ndani ya startimes.
FULL TIME : Simba 1 - 0 Rayon sports katika mchezo wa Simba Day.
DK 45 : Zimemalizika Simba 1 - 0 Rayon sports.
LWANDAMINA AJIUZULU RASMI ZESCO SASA MKUU PANDE MKUU SAWA NDANI YA YANGA SC,,,,,,,,,,,,,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
- quantalfaggart says:
Best Casinos in Las Vegas, NV - Mapyro
The best casinos in Las... more
Pageviews
66,321
No comments: