Posted by On the spot Tz
3:56:00 AM
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba amekiacha chama kwenye wakati mgumu baada ya kujiuzulu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Agosti, mwaka jana, Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kukabidhi barua kwa uongozi baada ya kushauriana kwa kipindi kirefu na viongozi na wazee wa chama hicho, akisema nafsi yake inamsuta kwa kuwa walikiuka malengo ya Ukawa.
Hata hivyo, hivi karibuni Profesa Lipumba aliandika barua ya kutengua uamuzi wa kujiuzulu na uchaguzi ulipoitishwa ili kujaza nafasi hiyo hakuchukua fomu ya kugombea.
Akizungumza katika mahojiano maalumu, Mtatiro amesema Profesa Lipumba amekitelekeza chama kikiwa katikati ya uwanja wa mapambano.
Mtatiro aliyeteuliwa hivi karibuni na Baraza Kuu la CUF kuongoza kamati ya uongozi wa chama hicho baada ya kuvunjika kwa mkutano mkuu ulioitishwa kuziba nafasi ya mwenyekiti, amesema walijaribu kila mbinu kumshauri Profesa Lipumba asijiuzulu bila mafanikio.
“Tukamuuliza kama ni kujiuzulu kwa nini usifanye baada ya uchaguzi? Kwa sababu wewe ndiye jemedari wa vita, wewe ndiye uliyeleta mabadiliko, wewe ndiye mwenyekiti wa Ukawa, sasa leo vita ndiyo inaanza umeshapeleka askari mstari wa mbele halafu unarudi nyumbani. Askari kule mstari wa mbele unamwachia nani?” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo Profesa Lipumba aliondoka na alituacha katika wakati mgumu sana. Kwa sababu sasa unamwachia chama Shaweji Mketo (Mkurugenzi wa Uchaguzi- CUF) aende kugawana majimbo na kina Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema), yule ni kijana, wale ni wazee…”
Alisema Profesa Lipumba alipoondoka CUF, heshima ya chama ilishuka kwa sababu hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa kujadiliana na viongozi wengine wa Ukawa na pia ilipoteza majimbo waliyoyatarajia kuyapata katika uchaguzi.
Aliongeza kuwa CUF ingeweza kupata zaidi ya majimbo 25 kama Profesa Lipumba angekuwapo, lakini yalichukuliwa na vyama vingine.
“Kwa hiyo kupata majimbo 10 ilikuwa ni kwa sababu ya kuondoka kwa Lipumba. Haya jemedari amekimbia vita, amesusa kwa sababu ya Ukawa. Lakini tulitarajia aende kunadi wagombea wake wa CUF, maana yeye ni mwanachama,” amesema Mtatiro.

Tagged with:
HABARI KITAIFA

On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
- quantalfaggart says:
Best Casinos in Las Vegas, NV - Mapyro
The best casinos in Las... more
Pageviews
66,431
No comments: