Posted by On the spot Tz
9:49:00 PM
0
Beki wa Yanga SC, Hassan Kessy aliyekosa penalti na kushuhudia Yanga ikifungwa kwa penalti 4-1 dhidi ya Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii, juzi alijikuta akibaki na mshangao kwa kile alichofanyiwa na Wanayanga mara baada ya mchezo huo.
Kessy ambaye alijua anaweza kupata lawama nyingi kwa kukosa penalti katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, anasema kuwa alipigiwa simu nyingi na mashabiki wa Yanga waliokuwa wakimfariji.
"Naomba niwaombe radhi Yanga kwa kukosa penalti, ukweli ni kuwa ile mechi tulitakiwa kuimaliza mapema kwa kuwa tulitawala mchezo huo lakini ndiyo hivyo.
“Nashukuru mashabiki wa Yanga kwa kunipigia simu kujifariji na kunitia moyo baada ya kukosa penalti, niwaambie kuwa tupo pamoja," alisema Kessy na kuongeza:
“Siwezi kuzungumzia sana namna nilivyokosa lakini najisikia vibaya kwa kweli, inaniuma sana.”
Aidha, akizungumzia kuhusu kumwaga machozi mara kadhaa katika mchezo huo, Kessy alisema: “Nalia kwa sababu ya furaha kwani sikuamini kabisa kama ningeitumikia Yanga kwa sababu kila mtu anajua nini kinachoendelea dhidi yangu.
“Tangu nimetua Yanga nimekumbana na vizingiti vingi sana ambavyo vimenifanya nishindwe hata kucheza mechi za kimataifa ila naamini Mungu yupo na kila kitu kitakaa sawa,” alisema.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: