Posted by On the spot Tz
2:57:00 PM
0
Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amesema kwamba
kitendo cha Rais Dkt. John Magufuli kusema kwamba siasa ziachwe hadi
miaka mitano iishe kunatokana na tabia ya upinzani kugomea kila kitu
bila kuweka maslahi ya taifa mbele.
Dkt. Mrema ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumzia kuhusu kauli hiyo ya Rais na kama haitaviathiri vyama kikiwemo chama anachokiongoza cha TLP.
''Kwa maoni yangu binafsi hii imetokana na tabia yetu sisi wapinzani kugomea kila kitu hata mambo ambayo yana maslahi kwa taifa, kwa mfano ukiangalia wakati Rais Dkt. John Magufuli anazindua bunge la bajeti wapinzani walimgomea na kutoka nje, hapa walianza kumhukumu kabla hajaanza kazi''- Amesema Mrema.
Mrema ameongeza kuwa hata bunge la bajeti linaloendelea wabunge wa upinzani wametoka vikao karibu vyote wakati bajeti inayojadiliwa siyo ya Naibu Spika ni bajeti ya serikali na kwamba wangetumia kanuni za bunge kuweza kumuondoa kama hawamtaki kuliko kuacha kuwakilisha wananchi wao.
Aidha Mrema ameenda mbali na kusema kuwa nchi hii haiwezekani kila siku ikawa ni maandamano kwani wananchi wanatakiwa wafanye kazi na kama wapinzani walikuwa na nia ya dhati wangebakia bungeni wajadili kwanza bajeti.
Kuhusu chama chake pia kutofanya siasa Mrema amesema yeye hana maandamano ya kila mara hivyo anaamini atakuwa na mikutano halali muda ukifika lakini kwa sasa wananchi wafanye kazi kwanza.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
HABARI KITAIFA

On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
- quantalfaggart says:
Best Casinos in Las Vegas, NV - Mapyro
The best casinos in Las... more
Pageviews
66,417
No comments: