Posted by On the spot Tz
12:50:00 PM
0
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeridhia uchaguzi wa Yanga uendeshwe na klabu yenyewe na utafanyika Juni 11, mwaka huu - jambo ambalo ni ushindi kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha pamoja baina ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na uongozi wa Yanga chini ya Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Clement Sanga.
Sanga ambaye amechukua fomu za kutetea nafasi yake, aliambatana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit kwa ajili ya kujadili mustakabali wa uchaguzi wa Yanga ambao uliingia katika mvutano na TFF pamoja na BMT.
"Maamuzi yaliyotoka ni kwamba, uchaguzi wa Yanga umebarikiwa kuendelea kama ulivyopangwa na kamati ya uchaguzi ya Yanga kwamba utafanyika June 11, 2016 chini ya uangalizi wa kamati ya uchaguzi ya TFF,"amesema Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas leo Dar es Salaam.
Lucas amesema kwamba wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo ambao walichukua fomu TFF, kikao kimeamua kiwarudishe kamati ya uchaguzi ya Yanga kuendelea na taratibu zilizopo za uchaguzi endapo wanakidhi vigezo vya uchaguzi vya kamati ya uchaguzi ya Yanga.
Mvutano uliibuka kuhusu uchaguzi wa Yanga SC kiasi cha kuwaacha njia panda wanachama wa klabu hiyo, wakiwa hawajui washike lipi, baada ya TFF kutangaza na kuendesha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo - wakati huo huo klabu hiyo nayo ikitangaza na kuendesha mchakato wake huo yenyewe.
Yanga ilisema uchaguzi wake utafanyika Juni 11 na na TFF ikasema utafanyika Juni 25. Na wote na zote zikaanza kugawa fomu za kugombea wiki iliyopita.
Waliochukua fomu TFF ni Aaron Nyanda, Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati miongoni mwa waliochukua fomu Yanga ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayoub Nyenzi.
Wakati mvutano huo, ukiendelea uongozi wa Yanga ukaibua tuhuma za TFF kwa kushirikiana na Kamati yake ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti, Wakili Alloyce Komba kupanga njama za kumkata Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
Kwa tuhuma hizo, mwishoni mwa wiki Wakili Komba alitangaza kujitoa kusimamia mchakato wa uchaguzi wa Yanga.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: