Posted by On the spot Tz
4:24:00 PM
0
Azam
FC imeamua kuachana na kipa wake mkongwe Ivo Mapunda waliyemsajili
msimu uliopita kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, huku
wakifanya mchakato wa kumsajili kipa mwingine.
Ivo
ambaye ni kipa mkongwe alitua Azam FC msimu uliopita akitokea Simba
baada ya kushindwa kumsajili katika dakika za mwisho ambapo
wanalambalamba hao waliamua kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Katibu
Mkuu wa Azam FC, Idrisa Nassor amesema kuwa, hawataendelea na Ivo msimu
ujao wa ligi kuu na kwa sasa wanafanya mchakato wa kusajili kipa
mwingine atakayeziba nafasi yake.
“Hatutarajii
kuendelea na Ivo msimu ujao wa ligi kuu na badala yake nafasi yake
itachukuliwa na kipa mwingine ambaye tunafanya mchakato wa kumsajili ili
kuziba nafasi hiyo.
“Kwa
sasa amebakiza miezi mitatu ili kukamilisha mkataba wake na Azam
aliosaini mwaka mmoja msimu uliopita na baada ya hapo tutaangana alisema
bosi huyo.
SOURCE: CHAMPIONI
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments: