Yoweri Museveni  Aaapishwa  Rasmi,,,,

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye alishinda katika uchaguzi wa mwezi Februari mwaka huu, Jana  Alhamisi ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tano mfululizo.
Sherehe za kuapishwa Yoweri Museveni ambazo zimefanyika jijini Kampala, zimehudhuriwa na marais wa nchi kadhaa za Afrika akiwemo Rais Omar al Bashir wa Sudan.
Museveni (71) aliingia madarakani mwaka 1986 nchini Uganda na katika uchaguzi wa tarehe 18 Februari mwaka huu, ameshinda kwa asilimia 60.62 ya kura.
Waangaliaji wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi wa Rais nchini Uganda ulifanyika katika anga ya vitisho na hofu iliyosababishwa na miamala mibaya ya serikali.
Daktari Kizza Besigye, mmoja wa wagombea wa upinzani amekataa matokeo hayo na kujitangaza mshindi.
Jana polisi wa Uganda walimtia mbaroni Dakta Besigye. Baada ya kukamatwa Besigye, chama chake cha FDC kilisambaza mikanda ya video katika mitandao ya kijamii, inayoonyesha kiongozi wao huyo akiapishwa kama rais wa Uganda na kusema kuwa kiapo cha leo cha Rais Museveni si halali.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply