Posted by On the spot Tz
1:11:00 AM
0
Kenya imetangaza kuanzisha tathmini kuhusu ni teknolojia ipi ya nyuklia itumike ili kujenga kinu cha nyuklia nchini humo.
Kaimu mkuu wa kitengo cha ufundi katika Bodi ya Umeme wa Nyuklia ya Kenya (KNEB) Bi.Winnie Ndubai ameliambia Shirika la Habari la Xhinhua kuwa, hadi sasa bado Kenya haijachagua teknolojia gani itatumika kwenye kinu kinachotarajiwa kujengwa, lakini kwamba ukubwa, usalama na maji ndiyo mambo yatakayozingatiwa wakati wa kujenga kinu hicho, na kusema teknolojia inayotafutwa ni ile inayoendana na mazingira ya Kenya.
Kenya inapanga kujenga kinu cha nyuklia kabla ya mwaka 2027, na tayari imesaini makubaliano na nchi kadhaa zenye teknolojia ya nyuklia ili iweze kuchagua teknolojia sahihi inayoweza kutumika.
Mwaka jana Kenya ililiomba Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA kufanya mapitio ya mpango wa Kenya kuhusu matumizi ya nyuklia.
KNEB inasema Kenya inahitaji kumiliki nishati ya nyuklia kwa sababu itamaliza vyano vya nishati ambayo huzalishwa kwa maji na mfuke katika kipindi cha miaka 20 ijayo.
Ndubai amesema nishati ya nyuklia ni yenye kutegemewa na itaiwezesha Kenya kuwa na uchumi wa masaa 24.
Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...


No comments: