De  Gea  Mchezaji  bora  Man  United,,,,

WASHINDI WA TUZO ZA MANCHESTER UNITED 

Mchezaji Bora wa Mwaka: David de Gea
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wachezaji: Chris Smalling 
Mchezaji Bora wa U-21: Cameron Borthwick-Jackson 
Mchezaji Bora wa U-18: Marcus Rashford
Bao Bora la Msimu: Anthony Martial v Liverpool   
Kipa wa Manchester United, David  De  Gea akipokea  tuzo  ya  mchezaji  bora  mbele  ya  kocha  wake  van  gaal.

WACHEZAJI wawili wa Manchester United, David de Gea na Chris Smalling wameng'ara katika tuzo za msimu za klabu hiyo inayofundishwa na Louis van Gaal.
De Gea ameshinda tuzio ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki wa klabu, wakati Smalling ameshinda Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la wachezaji wenzake katika sherehe zilizofanyika usiku wa Jumatatu Old Trafford.
Kipa wa kimataifa wa Hispania, De Gea amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu akiokoa michomo mingi ya hatari na kuisaidia United kubeba pointi.
Mshambuliaji kinda, Marcus Rashford ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa umri chini ya miaka 18, wakati beki Cameron Borthwick-Jackson ameshinda Mchezaji Bora kwa vijana chini ya umri wa miaka 21.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply