Posted by On the spot Tz
4:37:00 PM
0
Timu
ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuingia Dar es Salaam,
Tanzania kesho saa 7.45 usiku (usiku wa kuamkia Ijumaa Juni 24, 2016),
kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini
ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa
10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu
hiyo inaingia wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na
itafikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Waamuzi
wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya
timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti
Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo
huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse
Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw
Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku
mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa
ni Bester Kalombo.
Serengeti
Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa
kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa
Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na
Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika
kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako
walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA
(AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
WATOTO WA KAGAME WAITIKISA TIMU YA TAIFA YA RWANDA,,,,,,Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasi...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: