HAMIS  KIIZA

Uongozi wa klabu ya Simba umetupa macho zaidi kwa wachezaji kutoka Afrika Magharibi na kuamua kuachana kabisa na wale wanaotokea Kenya na Uganda.

Taarifa za ndani kutoka Simba, zimeeleza wameamua kufanya hivyo baada ya kukerwa na mambo mengi yaliyotokana na Waganda na Wakenya.

Msimu uliopita, Simba ilisajili Waganda watano, lakini Emmanuel Okwi na Juuko Murshid pekee ndiyo walifanya vizuri huku wawili wakigeuka mizigo.

Msimu huu, Juuko alianza vizuri, mwishoni akadorora. Hamisi Kiiza akafunga mabao 19, lakini mwisho uongozi wa Simba ukamshutumu kuwa ni tatizo kubwa miongozi mwao.

"Kweli tumeamua tuangalie wachezaji Afrika Magharibi, maana Wakenya na Waganda wamegeuka tatizo kubwa na hawakuwa na 'pafomensi' nzuri kwa kweli. Waliofanya vizuri ni Kipa Angban na Majabvi ambao wanatokea Ivory Coast na Zimbabwe.

"Mkenya Paul Kiongera alikuwa majeruhi na alipopewa nafasi hakuonyesha chochote. Juuko umeona alichotufanyia mwishoni, hakuwa msaada hata kidogo.

"Achana na hivyo, rejea kwa Kiiza. Kafunga mabao mengi kweli, alikuwa msaada awali. Lakini mwisho ndiye kawa tatizo, utaona hata kufunga hakuwa akifunga lakini sisi tunajua kila kitu na siku moja tutaweka mambo hadharani kabisa," alisema kiongozi huyo.

"Sasa tunajaribu kutafuta wachezaji wa Afrika Magharibi ambao watakuwa wapya kabisa hapa Afrika Mashariki ili tuweze kujenga kikosi chenye uaminifu."

Kikosi cha Simba kimemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya mabingwa Yanga, Azam FC wameshika nafasi ya pili.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply