Polisi ya Kongo DR yawashambulia waandamanaji wanaopinga kuahirishwa tarehe ya uchaguzi
Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewashambulia waandamanaji waliokuwa wanaandamana kupinga kuahirishwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Katika hujuma hiyo polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi sanjari na kuwatia mbaroni baadhi ya waandamanaji hao. Jean-Bosco Kalenga afisa wa ngazi za juu katika kikosi cha polisi amedai kuwa, polisi iliwashambulia waandamanaji hao kwa kuwa walikuwa wanahatarisha usalama wa nchi. Katika mji wa Lubumbashi, kusini mashariki mwa nchi hiyo, polisi pia imewashambulia waandamanaji wanaokadiriwa kufikia 5000, ambao walimiminika mabarabarani kupinga hatua hiyo ya kusogezwa mbele tarehe ya uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Waandamanaji walikusanyika mbele ya ofisi za Muungano wa Kitaifa wa Kifederali UNAFEC, za wapinzani wa serikali ya Rais Joseph Kabila. Kabla ya hapo, viongozi wa upinzani walikusanyika mbele ya ofisi za muungano huo mjini Kinshasa na kulaani hatua za rais huyo zilizo kinyume na demokrasia. Kwa sasa anga ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa tete kufuatia hatua ya kamisheni huru ya uchaguzi ya nchi hiyo kuahirisha uchaguzi mkuu, hatua ambayo inatajwa kuwa ni njama za kumsafishia njia Rais Kabila ya kuendelea kusalia madarakani. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Rais Joseph Kabila aliyeingia madarakani mwaka 2001, haruhusiwi tena kugombea uchaguzi ujao
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply