Posted by On the spot Tz
11:36:00 PM
0
Kocha George Lwandamina raia wa Zambia, yuko jijini Dar es Salaam.
Taarifa
zimeeleza kwamba kocha huyo ametua mchana na amewekwa katika moja ya
hoteli kubwa jijini Dar es Salaam, Yanga wakitaka kufanya siri kubwa.
Kamati ya Ufundi ya Yanga, imempendekeza kocha huyo kutua nchini na kuinoa Yanga badala ya Kocha Hans van der Pluijm.
Hata
hivyo, taarifa nyingine zimeeleza kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya
Pluijm ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga.
Bado kumekuwa na mkanganyiko kuhusiana na kocha huyo kwa kuwa Yanga wamefanya ni siri kubwa.
Lakini habari za uhakika zimeeleza, tayari Yanga wamemalizana naye licha ya kuwa wanafanya siri kubwa kuhusiana naye.
"Kila kitu kimemalizika, kocha yuko Dar es Salaam, mambo yanakwenda safi kabisa. Lakini vuteni subira," alisema mpasha taarifa.
Lwandami
alikuwa kocha bora wa Zambia msimu wa 2014-15, pia aliwahi kuinoa Zesco
ya Zambia kwa mafanikio makubwa, pia timu ya taifa ya Zambia maarufu
kama Chipolopolo.

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
UCHAGUZI MAREKANI WAPAMBA MOTO,,,,,Wagombea Urais marekani Licha ya ushindi wa Trump wa Jumanne ya jana kuzidi kumuhak...
No comments: