
Posted by On the spot Tz
10:08:00 AM
0

Leo Juni 05, 2016 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekaa katika kikao chake cha kawaida cha 18.
Kamati ya Utendaji imepitia taarifa mbalimbali za ligi na kukubaliana namna ya kuboresha mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes, Ligi Daraja la Pili pamoja na Ligi ya Mabingwa wa Mkoa.
Kadhalika kamati iliangalia uendeshaji wa Ligi za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambayo wiki iliyopita ilipata udhamini wa haki za kuonyeshwa kwenye televisheni kutoka kituo cha televisheni cha Azam.
Pia Kamati ya Utendaji imepitisha azimio la kanuni ya leseni ya klabu kuwa ni lazima ianze kutumika msimu mpya wa mashindano wa 2016/17.
Mahitaji ya kanuni hiyo ni pamoja na klabu kuwa na Watendaji wa kuajiriwa kama vile Katibu Mkuu (GS), Mkurugenzi wa Ufundi (TD), Ofisa Usalama (Security Officer) na taarifa ya fedha zilizokaguliwa pamoja na Meneja wa Fedha ambaye atakuwa na uwezo wa kuandaa taarifa za fedha zitakazokaguliwa na wakaguzi wa mahesabu.
Pia klabu zinatakiwa kuwa na ofisi, Uwanja wa mazoezi, kuendeleza program ya vijana ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kusoma na na kwamba hakuna mmiliki mmoja anayeruhusiwa kuwa na timu zaidi ya moja katika ligi.
Pamoja na hayo Kamati ya Utendaji iliteua wajumbe wa kamati mbalimbali za kawaida na za kisheria. Orodha kamili ya kamati hizo hii.

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: