Posted by On the spot Tz
9:53:00 AM
0
AMISI JOSLYN TAMBWE.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameushauri uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unasajili kiungo mkabaji (namba sita), wa nguvu katika kipindi hiki cha usajili ambaye atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao 21, amesema Yanga inakabiliwa na tatizo kubwa la kiungo mkabaji mwenye uwezo kupambana muda wote wa mchezo.
Alisema hali hiyo ndiyo imekuwa ikiisumbua timu hiyo katika mechi zake za kimataifa jambo ambalo uongozi wa timu hiyo unapaswa kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili.
“Tuna viungo wengi wazuri lakini bado tunahitaji kiungo mkabaji wa nguvu ambaye atakuwa anashirikiana vilivyo na mabeki wetu katika safu ya ulinzi.
“Uongozi wetu unatakiwa kuliona hilo na kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili kabla ya kuanza kushiriki michuano ya kimataifa ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya timu tutakazokutana nazo,” alisema Tambwe
onthespottz.blogspot.com
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: