Posted by On the spot Tz
12:50:00 PM
0
Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara Mrundi, Amissi Tambwe amewatoa hofu mashabiki wa Yanga, akiwaambia: “TP Mazembe kitu gani, lazima wakae.”
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa siku chache tangu Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kufanya droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa Yanga ku
pangwa Kundi A na Timu za MO Bejaia (Algeria), Medeama (Ghana) na TP Mazembe huku Kundi B, likiwa na Kawkab (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia), FUS Rabat na Ahly Tripoli ya Libya.
Mrundi huyo, kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara ameweka rekodi ya pili ya kuchukua ufungaji bora kwenye ligi akifunga mabao 21 huku akiwapita Hamis Kiiza mwenye mabao 19 na Donald Ngoma aliyefunga mabao 17.
Tambwe alisema soka la Afrika limebadilika kwa kiwango kikubwa, hivyo haoni sababu ya kuwahofia wapinzani wao Mazembe.
Tambwe alisema, katika kuthibitisha hilo, wamepanga kushtusha watu kwa kuwaondoa Mazembe na kutwaa ubingwa huo, mwaka huu na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chao.
“Ni mbaya kuishi kwa mazoea kama ilivyokuwa kwa Mazembe ambao wanapewa nafasi kubwa ya kututoa kwenye hatua ya makundi Afrika kitu ambacho siyo sahihi.
“Nikuhakikishie tu, soka la Afrika limebadilika kwa kiwango kikubwa, hao Mazembe wanaopewa nafasi kubwa ya kututoa, niamini tunawatoa wao na kuchukua ubingwa huo na kama unabisha subiria uone.
“Hayo ndiyo malengo tuliyojiwekea na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chetu kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu wa michuano hiyo,” alisema Tambwe.

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: