Posted by On the spot Tz
8:37:00 AM
0
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta(pichani) hataweza kusafiri na Taifa Stars kwenda Nairobi, Kenya kucheza na wenyeji Harambee Stars mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
KRC Genk imemuombea Samatta kutorejea nchini kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu inamuhitaji katika mechi ya mchujo wa mwisho wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Europa League.
Na kwa ombi hilo la timu hiyo ya Ubelgiji, Samatta hatakuwemo kwenye msafara wa unaoondoka kesho saa 12.00 Alfajiri chini ya makocha wake, Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei 18, 2016 mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unadumisha uhusiano na upendo wa enzi wa nchi za Kenya na Tanzania na umeingizwa kwenye orodha ya viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Kikosi cha Stars kina makipa, Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Mwinyi Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
No comments: