Posted by On the spot Tz
9:14:00 AM
0
Jerry Silaa
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) amedai kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtishia kuchoma moto nyumba yake wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.Silaa alieleza hayo jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati akitoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara (Chadema).
Alitoa ushahidi huo kwa njia ya kiapo baada ya Jaji Fatuma Msengi kutupilia mbali pingamizi la upande wa walalamikiwa waliokuwa wanapinga kupokewa kwa kiapo hicho kwa kuwa kina mapungufu kisheria.
Katika kiapo hicho, Silaa anaeleza kuwa, Oktoba 27 mwaka jana katika kituo cha kujumlishia kura cha Pugu Sekondari, kulikuwa na idadi kubwa ya wapiga kura wa Chadema wakiwa wamesimama mita 20 kutokea usawa wa kituo hicho.
Alidai kuwa wafuasi hao walianza kuwatishia Mawakala na Msimamizi wa Kituo, jambo lililosababisha Polisi washindwe kufanya kitu zaidi ya kuwaonya, ndipo mjibu maombi wa pili na wenzake wakasema hawatopokea matokeo na watachoma moto nyumba yake pamoja na kituo hicho.
Silaa ambaye aliwahi kuwa, Meya wa Manispaa ya Ilala, alidai hadi Oktoba 27, baadhi ya vituo vilikuwa havijakusanya matokeo jambo lililosababisha aandike barua kwenda kwa Msimamizi wa Kituo kuomba mchakato wa kuhesabu kura urudiwe.
onthespottz.blogspot.com
Tagged with:
HABARI KITAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam,,,,,,,Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za b...
-
Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star, Jijini Dar Baada ya Kukutwa Kimejaa Makopo ya MIKOJO na KINYESIUKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako w...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: