Polisi nchini Kosovo imemtia mbaroni kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki anayedaiwa kuwanajisi watoto wadogo katika taasisi moja ya kidini nchini Uingereza na kisha kutoroka nchi.
Veton Elshani, Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Ushirikiano wa Kimataifa cha Kosovo amesema kasisi huyo wa Uingereza kwa jina Andrew Charles Kingston Soper alikamatawa akiwa mafichoni katika mji wa Peja, mashariki mwa nchi. Amesema kuwa kasisi huyo amekamatwa kutokana na waranti iliyotolewa na serikali ya London mwaka 2011.
Idara ya Mashtaka ya Umma nchini Kosovo imeagiza kuendelea kuzuiliwa kasisi huyo mtoro hadi mahakama ya nchi hiyo iamue iwapo atarejeshwa nchini Uingereza au la.
Kingston Soper ambaye pia anafahamika kama Father Laurence, anadaiwa kuwanajaisi watoto watano ambao walikuwa wanafunzi wake katika shule binafsi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki ya St. Benedict’s, katika kitongoji cha Ealing Abbey magharibi mwa mji mkuu wa Uingereza, London.
Haya yanajiri siku chache baada ya Dayosisi Kuu ya Kanisa Katoliki katika mji wa Baltimore jimboni Maryland nchini Marekani kufichua majina ya makasisi 71 wanaotuhumiwa kuwalawiti watoto wadogo.
Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Marekani, takriban makasisi 6,900 wa Kanisa Katoliki la Roma wanadaiwa kuwalawiti watoto wadogo 16,900 kati ya mwaka 1950 na 2011.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply