Posted by On the spot Tz
8:15:00 AM
0
Rais Omar al-Bashir wa Sudan aliwasili nchini Uganda hapo jana Alkhamisi kwa lengo la kufanya mazungumzo na vilevile kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.
Bashir ameelekea nchini Uganda katika hali ambayo ni muda mrefu sasa tokea uhusiano wa nchi mbili hizo uharibike. Sudan inaituhumu Uganda kwamba inawapo hifadhi waasi wa Sudan kutoka majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile ambao wanapigana na serikali ya Khartoum. Khartoum vilevile inaituhumu serikali ya Kampala kwamba inawapa hifadhi waasi ambao waliandaa mazingira ya kujitenga Sudan Kusini na Sudan mwaka 2011. Kwa upande wake Kampala nayo inaituhumu Khartoum kwamba inawapa hifadhi na silaha waasi wa Lord's Resistance Army ambao wamevuruga hali ya amani na usalama kaskazini mwa Uganda. Hata hivyo safari ya Museveni mjini Khartoum mwezi Septemba uliopita ilisaidia pakubwa kupunguza mvutano uliopo kati ya nchi hizo. Katika safari hiyo viongozi wa nchi mbili hizi walitiliana saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano katika njama za usalama, kupambana na ugaidi na uhalifu ulioratibiwa, magendo ya binadamu, kuimarisha kamati ya pamoja ya kushughulikia masuala ya usalama na kutekelezwa ratiba za kijeshi katika taasisi za pande mbili. Katika hali ya hivi sasa inaonekana kuwa kuchunguzwa kwa hali ya Sudan Kusini ndiko kumepewa kipaumbele katika mazungumzo ya viongozi hao. Sudan daima inaituhumu Uganda kuwa inafanya juhudi za kutaka kudhibiti hali ya mambo nchini Sudan Kusini. Mvutano wa nchi mbili hizi ulifikia kilele wakati wa kujiri mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na wa makamu wake aliyeuzuliwa Riek Machar mwaka 2913, ambapo Uganda ilimuunga mkono waziwazi Salva Kiir. Wakati huohuo kuwekwa askari wa Uganda katika mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Sudan Kusini kulizidi kuiweka wasiwasi serikali ya Sudan. Wajuzi wa mambo waasema kuwa suala la Nile ndilo limeipelekea serikali ya Kampala kujikurubisha kwa Sudan. Mwaka 1999, nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Sudan, Kenya, Rwanda na Uganda zilitia saini mkataba wa 'Uvumbuzi wa Serikali za Eneo la Nile.' Nchi hizo zimefanya vikao kadhaa baada ya kuzuka mvutano baina yao na vilevile kupungua kwa kiwango kikubwa maji ya Mto Nile. Hatimaye Mkataba wa Kampala ulitiwa saini mwaka 2010 ambapo nchi shiriki ziliafikiana kuainisha mfumo wa kushirikiana na kurekebisha mkataba wa zamani kuhusiana na matumizi ya maji ya mto huo. Katika mkataba huo wa Kampala nchi za Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na uganda zilitajwa kuwa nchi zilizo kwenye eneo la chanzo cha Mto Nile nazo Misri na Sudan ambazo zilitajwa kuwa eneo la mwishoni mwa mtu huo zikakataa kuutia saini kwa hoja kuwa haki zao hazikuzigatiwa. Hata hivyo nchi mbiili hizo baadaye zililazimika kuutia saini kutokana na mashinikizo ya nchi zilizoutia saini na pia ya nchi nyingine za nje ya mkataba huo.
Tagged with:
KIMATAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...


No comments: