Posted by On the spot Tz
5:45:00 AM
0
Jerry Muro
Klabu ya Yanga kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Muro, wamesema wako tayari kuisaidia Simba kulipa deni la Musoti ili klabu hiyo ya Msimbazi isishushwe daraja.Muro amsema, wako tayari kuichangia Simba kulipa deni lao linalowakabili ili FIFA isiishushe daraja na wao wakakosa pointi sita katika msimu ujao wa VPL.
“Tunaomba watuletee barua na karatasi za malipo za yule mchezaji ili sisi tu-process malipo kwa sababu tuliahidi tukifika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika tutawasaidia kulipa deni lao. Sisi hatukubali Simba ishushwe daraja kwasababu pale tunapointi sita za wazi kwenye msimu ujao wa ligi”.
“Sasa kwanini tukose pointi sita ambazo tunaweza tukazitetea zikabaki. Inaweza ikashuka Simba halafu ikapanda timu ya Milambo ya Tabora halafu ikatusumbua sana, sisi tunazihitaji ponti sita za Simba na tulisema tukifika hatua ya makundin tutawalipia”.
“Ili tuweze kufanya transaction na kwakua hela hii inalipwa kupitia FIFA, tutawaandikia CAF barua ya kufanya malipo kwenda FIFA ili kuisaidia Simba isishuke daraja. Mhasibu wetu anasubiri karatasi za malipo na kwakua malipo yanafanyika kwa dollar, tutawaandikia CAF watoe kiasi cha pesa kwenda FIFA kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu”.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
onthespottz.blogspot.com
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: